Jumamosi , 30th Jul , 2016

Baraza la sanaa Tanzania BASATA limesema shindano la Dance100% ni kielelezo kizuri katika ukuaji wa sanaa kwa kukuza urafiki na maelewano ya vijana ndani ya jamii

Mkuu wa Matukio ya Sanaa kutoka BASATA Bwn. Kurwijira N Maregesi

Akizungumza na EATV katika viwanja vya TCC Chang’ombe , Mkuu wa matukio ya sanaa kutoka BASATA Bwn. Kurwijira N Maregesi amesema Baraza la sanaa nchini linafurahishwa sana na namna ambavyo EATV inaibua vipaji vya vijana mbalimbali hapa nchini kupitia mashindano mbalimbali likiwemo la Dance100%.

‘’Shindano la Dance100% linakua kila iitwapo leo na vijana wengi waliopo mikoani wanapata fursa ya kutizama wenzao wanachokifanya na undugu na ushirikiano vimezidi kukua baina ya vijana kupitia shindano hili'' .Amesema Bwn. Maregesi.

Maregesi ameongeza kuwa licha ya shindano hilo kutoa fedha pia ni fursa pekee kwa vijana kuweza kujenga afya kutokana na mazoezi ambayo vijana wanafanya kujiandaa na usaili.

Aidha ameshauri kwamba shindano kwa miaka ijayo liangalie namna ya kufanya usaili mikoani kwani mwitikio wa vijana kuhusu shindano hilo ni mkubwa sana.

Tags: