
Katika mahojiano ya hivi karibuni, Davido alieleza kuwa alipanga kufanya wimbo mmoja tu, ambao kama ungeweza kusikika redioni hata mara moja au mbili, basi hilo lingemtosha kabisa. Hakuwa na ndoto kubwa ya kuwa nyota wa kimataifa, bali alitaka tu kujaribu bahati yake katika muziki.
“Mimi nilikuwa nataka tu kusikia wimbo wangu redioni, hata kama ni mara moja tu, ningeridhika,” alisema Davido
Lakini mambo yalibadilika haraka. Wimbo wake wa kwanza ulipopata mapokezi makubwa, safari yake ya muziki ilianza rasmi,safari ambayo imekuwa ya mafanikio makubwa na ya kusisimua duniani kote.
Cha kushangaza zaidi, Davido hakuingia studio kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kurekodi kazi yake binafsi. Alikuwa akisindikiza binamu yake kwenda kurekodi wimbo, ndipo akajikuta akiingia mwenyewe kwenye muziki.
“Nilikuwa naenda studio kumsindikiza binamu yangu... Sikutegemea kabisa kuwa maisha yangu yangebadilika hivyo,” aliongeza.
Kwa sasa, Davido ni mmoja wa wasanii wakubwa Afrika na duniani kote, akiwa na tuzo nyingi, ushawishi mkubwa, na mamilioni ya mashabiki.