Jumapili , 9th Apr , 2017

Msanii wa bongo fleva Dayna Nyange amesema mwanamitindo Daxx Cruz ambaye walikuwa naye kwenye show moja Jumamosi iliyopita ni rafiki yake wa kawaida na hawana mahusiano yeyote.

Akipiga story kupitia eNewz Dayna  amesema Daxx ni rafiki yake wa karibu tangu siku nyingi na wamekuwa wakishauriana mambo mbalimbali na hata wakati mwingine wamekuwa wakipeana kampani kwenye mambo mbalimbali hali inayopelekea kuwafanya watu wawahisi kwamba ni wapenzi

Hata hivyo Dayna amesema yeye na Daxx wanaelewana sana na ni mtu ambaye amekuwa akimshauri hata anapokuwa na mawazo na ni mmoja kati ya watu wanaomfanya ajisikie vizuri kwenye maisha yake lakini hawana mahusiano ya kimapenzi.

Dayna amesema "Daxx ni mtu ambaye nimekuwa naonekananaye sehemu mbalimbali na huwa ninapokuwa na Daxx napenda kujiachia na kudeka japo huwa nina mipaka yangu kwa Daxx". 

Dayna alimalizia kwa kusema itafikia wakati atamuonesha mpenzi wake kwani hakuna namna.