Alhamisi , 19th Jun , 2014

Msanii aliyewahi kuliimbia kundi maarufu la muziki nchini Kenya 'Tattuu' Debbie Asila, baada ya muda mrefu kutokuwa katika gemu hivi sasa amerudi tena kuendeleza kipaji chake katika luninga.

Msanii wa muziki nchini Kenya Debbie Asila

Debbie ambaye ameliimbia kundi hilo kwa muda mrefu amerudi kwa kuanza kujitengenezea wigo kwa kukusanya mashabiki wake upya huku akiamini kufanya kazi ya utangazaji wa kipindi katika Televisheni kitalirudisha upya kundi lake la awali.

Macho yote yanamwelekeza msanii huyo wa kike aliyejijengea jina kubwa katika gemu ya muziki nchini Kenya.