Joozey
Akiongea kupitia eNewz Joowzey amesema kwa sasa kuna wasanii wawili kutoka Nigeria na mtayarishaji mmoja ambao anafanya nao kazi na atakapowekana nao sawa ataweka wazi ili watanzania wote wajue anafanya kazi za aina gani kwa sasa.
Pia Joowzey amesema kwa sasa muziki wa Tanzania unafanya vizuri kiasi kwamba kuna wasanii wa Nigeria wanatamani kuja kufanya kazi na waongozaji wa hapa nchini na kwa sasa Hansscana, Khalfani na Msafiri wanafanya vizuri kuliko hata huko South wanapokimbilia baadhi ya wasanii wetu.