Dorah ataja jinsia ya mtoto wa Tausi

Jumatano , 8th Jan , 2020

Msanii wa filamu nchini Dorah, amempongeza rafiki yake Tausi baada ya kujifungua salama na amesema, mtoto huyo atakuwa wa kwao wote na watahangaika naye.

Wasanii wa filamu upande wa kushoto ni Dorah, kulia Tausi

Akifunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, Dorah amesema anafurahi sana kwa Tausi kujifungua salama pia amejistiri na kujiepusha kutoonekana mitandaoni mpaka alivyojifungua.

"Kiukweli kutoka moyoni nimefurahi na nampongeza sana kwa kujistiri na kutojiweka katika mitandao mpaka amejifungua salama, angekuwa mwanamke mwingine angeenda kupiga picha 'photoshoot', maana hawashindwi si unajua tena ukiwa na mimba ya kwanza" amesema Dorah.

Aidha Dorah ameongeza kwa kusema "Tutamlea mtoto wetu na hatahangaika peke yake, maana sisi shangazi tupo wengi asijali tutampambania, ila siwezi nikamtaja baba ni nani maana hayo ni makubaliano ya wawili"

Tausi amejifungua mtoto wa kike siku ya Januari 8, 2020, ambapo kupitia mtandao wa Instagram, ameandika anamshukuru Mungu kwa kuwa amemfurahisha pia anajivunia kuwa mama