Jumatatu , 29th Jan , 2024

Huwenda duniani itachelewa kumuelewa hayati Remmy Ongala pale alipotamani kufahamu muziki asili yake wapi?

‘’Muziki asilia yake wapii eeenh..
Muziki ni wa nani eeenh...’’

Turudi nyuma mpaka mwaka 2013, Pale ambapo Samaya na Brother K kutokea ‘’kwanza Unit’’ (KU) walipoamua kubadili mtazamo wa Nikki Mbishi kwa kuonesha kuwa kile alichofanya hakipaswi kuwa kwenye udogo

Kwani wazo la Nikki Mbishi ni kuwa aitoe kama Mixtape, lakini kwakuwa ujazo ulikuwa ni mkubwa ikabidi ipendekezwe kutoka kama Album, ndipo mtazamo wa Nikki mbishi ukabadilikana na kuibatiza kuwa album, Ikafanyika kuwa album yake ya kwanza kuitoa akiwa kama msanii anayejitegemea.

Ndipo ikaachiwa rasmi album iliyopewa jina la Malcom wa 11 (Malcom XI), Na jina la Album limetokana na mapenzi yake kwa Malcom X, Malcom pia ndiyo jina la mtoto wake wa kwanza - Nikki mbishi Via Fanisi Tv

Sasa ndani ya Album hii kuna nyimbo nyingi lakini ipo inayohoji kuhusu Dunia bila ya uwepo wa muziki,

Kusingekuwa na muziki ndiyo maisha yangekuwepo,
Siri zingekuwepo ila mengi yangejificha,
Maarufu angevuma na kuondoka kama upepo,
Hata studio zingekuwepo lakini za wapiga picha,

Swali kwako mdau umewahi kujiuliza maisha ya mwanadamu yangekuwaje iwapo kusingekuwa na muziki?