Esha Buheti afunguka kuhusu ajali aliyoipata

Jumanne , 14th Jan , 2020

Msanii wa filamu na mfanyabiashara Esha Buheti amesema anasikitika sana kwa habari zianazoendelea kuhusu ajali aliyoipata pia yupo tayari kuongea na waandishi wa habari juu ya suala hilo pamoja na issue ya utapeli.

Gari ambayo amepata nayo ajali Esha Buheti

Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Esha Buheti amepost picha ya gari ambayo amepata nayo ajali katika daraja la Wami mkoani Tanga ambapo ameandika "Ahsanteni kwa  message zenu na simu nyingi sana nimezipata ila kwa sasa kicha kinauma sana, ni kweli tumepata ajali ila tumetoka salama alhamdulillah"

Aidha muda mfupi uliopita kupitia mtandao huohuo wa Instagram amepost video fupi ya gari alilopata nalo ajali likiwa limebebwa na kuandika,

"Tunaanza safari ya kurudi Dar, nasikitika sana kwa habari zinazoendelea kuhusu ajali hii, nimekaa kimya sana ila muda wa kuongea umefika, nimechoka kwenye maisha yangu sijawahi kumtapeli  wala kumuibia mtu"  ameandika

Mimi sio mtu wa maneno maneno ndiyo maana kwenye maisha yangu nipo kivyangu na kazi zangu, nimekaa kimya sana ila imezidi mara naishi maisha ya uongo, mara nimemkuwadia mtu mwanaume na nipo tayari kuongea na waandishi wa habari muda wowote" ameongeza