Ijumaa , 1st Oct , 2021

Mrembo Fahyma 'Fahyvanny' anasema bado anaendelea kumsifia baba mtoto wake Rayvanny kwa sababu ni mtu aliyekamilika na muhimu sana kwa upande wake.

Picha ya msanii Rayvanny na Fahyma

Fahyvanny ameeleza hilo akimjibu shabiki baada ya ku-comment kwenye picha aliyopost Instagram kwa kuandika "Kiboko yako Paula, kajua kukukomesha coz ulijimwamba fai sana mwanaume asifiwi wewe".

Fahyvanny akaijibu comment hiyo kwa kuandika "Bado naendelea kumsifia he so perfect to me sijui kwa wengine ila kwangu bado ni mtu muhimu sana, sababu roho ya mtoto wangu ni yangu pia".

Kwenye mahusiano yao wamepata mtoto mmoja ila kwa sasa wameachana baada ya Rayvanny kuwa kwenye mahusiano na Paula mtoto wa Kajala na P Funk Majani.