Ijumaa , 16th Sep , 2016

Fainali za Shindano la Dance100% linaloendeshwa na kituo cha EATV zinatarajiwa kufanyika Septemba 24 2016 katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es Salaam.

Kundi la Makorokocho

Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo mratibu wa shindano hilo Bhoke Egna amesema maandalizi yanaendelea vyema ambao katika shindano hilo mshindi mmoja ataibuka na kitita cha milioni 7 kama zawadi.

“Tunatarajia kufanya fainali za shindano letu Septemba 24 ambapo pamoja na kazi nzuri inayotarajiwa kuoneshwa na washiriki wetu vilevile kutakuwa na zawadi maalum kutoka kwa mashabiki watakaofika viwanjani kwa kujibu maswali na kuzawadiwa zawadi na wadhamini wa shindano Vodacom pamoja na Coca –Cola hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi” Amesema Bhoke.

Shindano la Dance100% linaoneshwa na EATV pekee kila Jumapili saa moja jioni ambapo matukio yote kutoka kwa washiriki yataonyeshwa.

Tags: