Haitham Kim amvaa tena Amber Lulu

Jumapili , 22nd Mar , 2020

Mrembo Haitham Kim amefunguka na kusema Amber Lulu ni mshamba na hana hadhi ya kutembea na mwanaume wake kwa sababu haendani naye.

Kushoto ni Haitham Kim, kulia Amber Lulu

Haitham Kim amesema hivyo baada ya kuwepo na stori zinazoelezwa kuwa Amber Lulu amemuibia mwanaume wake aitwaye Boshen, kisha kujirekodi wote video na kupost katika mtandao wa Instagram.

"Amber Lulu hawezi kunichukulia mwanaume wangu hana hiyo hadhi, ukimuangalia mpenzi wangu Boshen na Amber ni vitu viwili tofauti, aliamua kufanya ushamba tu wa kujirekodi video na kupost instagram na kuandika vitu anavyovijua yeye na sipendi kumuongelea maana nitampa kiki" amesema Haitham Kim.

Zaidi endelea kutazama hapa kwenye video hapa chini.