Jumatatu , 26th Apr , 2021

Msanii wa filamu Love Juakali amesema anachukizwa na vitu hasi 'negativity' na comments mbaya kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu watu hawajui nyuma ya pazia kuna mambo gani yanayomuhusu.

Msanii Love Juakali

Love amesema hivyo kufuatia baadhi ya mashabiki zake ku-comment suala la kumtaka afanye mazoezi na kupungua mwili wake kwenye mtandao wa Instagram, ambapo kupitia EATV & EA Radio Digital amesema hawezi na atamani kupungua na watu wasitarajie hilo.

"Sipendi 'negativity' na 'bad comments' mtu hajui vitu vinaanzia wapi yeye anakuja ku-comment bila kujua nyuma ya pazia, unaweza uka-post picha mtu anasema 'dada fanya mazoezi upungue' kwani lini nimewahi kuwaambia kwamba nataka kupungua au kuutamani wembamba, suala la kupungua wasahau" 

"Hamtokuja kuniona kuwa mwembamba na sijawahi kuwa hivo tangu nimezaliwa mpaka kufikia hapa, mtu akiona anachukizwa na mwili wake ndio afanye mazoezi ya kupungua ila sio kwangu tena mtanisamehe mimi siwezi kupungua kuwa mwembamba" ameongeza Love Juakali  

Mengine zaidi aliyoyasema Love Juakali tazama hapo chini kwenye video.