Msanii Duma
Akizungumzia kuhusu muonekano Duma ameeleza, "Ukishakuwa msanii lazima uwe na muonekano ambao utamvutia kila mtu usiangalie tu mwanamke, unajua kuna muda hata Boss mwenye kampuni au mwenye matangazo anaweza akavutiwa hata na mwili wako ili kufanya naye tangazo kwa hiyo ukiwa msanii ni vizuri ukatengeneza mwili wako uwe bora zaidi".
Duma ameendelea kusema hata asingekuwa msanii au staa bado angepata watoto wazuri kutokana na muonekano wake ila hicho sio kitu cha msingi sana kwa sababu hajakipa kipaumbele kwenye maisha yake huwa anawaza kazi mapenzi baadaye.
Kuhusu kufanya mapenzi amesema sio kama hana mpenzi na juzi tu wametoka kufanya, ila anaheshimu kwa sababu haijawa rasmi hawezi kuzini halafu atangaze mitandaoni wala hawezi kumpost mpenzi wake mitandaoni, hadi afikie hatua ya kumvalisha pete au ndoa.
