Ibraah amkana mrembo Nanah aliyemchora tattoo

Jumatatu , 3rd Mei , 2021

Ni 'headlines' za msanii Ibraah kutoka Konde Music Wordwide ambaye amekana kuwa kwenye penzi na msanii wa filamu na video vixen Nanah aliyechora tattoo yenye jina lake shingoni.

Kushoto ni msanii Ibraah na mrembo Nanah, kulia ni tattoo aliyochorwa Ibraah

Akizungumzia hilo kupitia Kamera ya EATV & EA Radio Digital, Ibraah amesema kuchorwa tattoo na mrembo huyo haihusiani kwamba ndio wapo kwenye mahusiano bali kilichokuwepo kwao ni upendo na urafiki.

"Nanah sio mtu wangu ni rafiki yangu na ana mahusiano yake, kuhusu tattoo kila mtu anaamua kuchora, nilivyomuona nilimuuliza akasema amependa tu kuchora jina la Ibraah kwa sababu mimi ni mtu wake wa karibu na nina umuhimu kwake, mbona kuna watu wengi wamenichora ila wanamsema Nanah tu" amesema Ibraah 

Pia ameendelea kusema urafiki wao kwa sasa una muda wa miezi 6 na kinachoendelea kati yao ni upendo tu.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.