Jay Moe aeleza kinachomsumbua kwenye muziki

Ijumaa , 31st Mei , 2019

Msanii wa Bongofleva Jay Moe, ameeleza kuwa huwa hasumbuliwi na mambo ya 'views' za ngoma zake kwenye mtandao wa Youtube ila anachozingatia yeye ni ujumbe utagusa wangapi.

Jay Moe

Akiwa kwenye DADAZ ya East Africa Television leo, Jay Moe amefunguka kuwa, wasanii kwasasa wanasumbuliwa na idadi ya watazamani wa Youtube na sio ujumbe utawagusa watu wa jamii ambao hata hawajui mambo ya mtandaoni.

''Siangalii wimbo unapata views ngapi kikubwa ni 'content' gani inakwenda kwa jamii, unakuta ngoma yangu haijapata watazamaji wengi kwenye Youtube, lakini unakwenda sehemu za ndani ndani unakutana na mtu anakwambia anakufuatilia na ana wimbo wako'', amefunguka.

Upande mwingine Jay Moe amesema kumekuwa na mambo mengi kwenye muziki na wasanii unakuta wanachukiana kisa hajapostiwa kwenye mtandao jambo ambalo sio la msingi sana.