Jaydee atoa siri kubwa kwenye maisha yake

Jumanne , 30th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkongwe kwenye game, Judith Wambura 'Lady Jaydee', ametoa siri ya kutozeeka haraka kunakomfanya kubaki na mwili wake wa ujana.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jaydee amesema kwamba sababu kubwa ya yeye kutozeeka ni kutokana na kula vyakula vyenye afya, na kuacha vile vyenye madhara.

Jaydee afunguka 

“Mimi sili nyama nyekundu, n'gombe, mbuzi, kitimoto sijui, pia sinywi soda, mara nyingi huwa nakula mboga mboga na white meat (samaki, kuku)”, amesema Jaydee.

Jaydee amekuwa mmoja ya wasanii ambao wameweza kukaa kwenye game kwa muda mrefu na kubaki kama walivyo, huku mwenyewe akisema kwamba hata nguo alizovaa kwenye album yake ya kwanza ya 'machozi', mpaka sasa bado zinamtosha.