Jumatatu , 23rd Sep , 2019

Mrembo na mfanyabiashara kutokea nchini Uganda, Zari 'The Boss Lady', ameonyesha jeuri ya pesa kwa kujizawadia nyumba nchini Afrika Kusini katika kumbukumbu ya kusheherekea miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake.

Zari 'The Boss Lady'

Imekuwa siyo kawaida kwa mtu kujizawadia mwenyewe jambo fulani lakini hii imetokea kwa Zari ambaye alipost picha katika “Insta Story” ya mtandao wa kijamii wa Instagram akionyesha mjengo huo.

Pamoja na mjengo, Zari pia aliandika, “ahsanteni kwa wote ambao mmeniletea zawadi kuelekea “birthday” yangu, nimejizawadia mwenyewe nyumba mpya, nashukuru kwa baraka za kuona naongeza mwaka mwingine, sina cha kukulipa M/mungu ahsante kwa neema zako”.

Zari ambaye ni mama wa watoto watano siku ya leo anatimiza umri wa miaka 39 ambapo jana aliandaa sherehe fupi ya chakula na vinywaji akiwa na ndugu, jamaa na marafiki zake nchini Afrika Kusini.

Wiki iliyopita Zari akiwa Jijini Dar Es Salaam pia alionekana katika studio za msanii Switcher Baba “Quick Rocka” ikionyesha kama wanarekodi wimbo.