Jinsi Majani alivyombadilisha Harmorapa

Friday , 21st Apr , 2017

Msanii Harmorapa amekiri kuwa mtayarishaji mkongwe wa muziki Bongo P Funk Majani ndiye amembadilisha kutoka kwenye uimbaji wa rap wa kizamani hadi kufikia kurekodi kiboko ya mabishoo ambayo inaendana sawa na soko la muziki wa sasa.

Harmorapa na P Funk ndani ya FNL

Akiwa Kikaangoni Harmorapa amesema kuwa baada ya kutoa ngoma ya kwanza 'Usigawe pasi' Majani alimtafuta na kumpongeza kuwa anajua kuandika lakini bado uimbaji ni wa kizamani hivyo akaanza kumtengeneza ili kukaa sawa.

"Unajua Majani ni legend producer hapa nchini. mimi alinitafuta nilipoachia tu ngoma ya kwanza usigawe pasi akaniuliza vipi, nikasema nina ngoma zingine nilizowahi kurekodi nikamsikilizisha. Alinipongeza  kwenye uandishi kwamba najua kuandika ila tatizo lipo kwenye rap yangu kuwa ilikuwa ya kizamani sana na kwamba muziki ni biashara, akaniambia kilichobaki kwangu ni training tu ili nifanye poa"- Harmorapa.

Amesema baada ya ushauri na maelekezo kutoka kwa Majani, nipo aliporekodi Kiboko ya Mabishoo, pamoja na ngoma nyingine ambazo amesema zinatoka muda si mrefu, akiwa amebadilika kabisa.