Jumatatu , 19th Mei , 2014

Msanii wa muziki kutoka Sudan Kusini, K-Denk ambaye alijipatia umaarufu kupitia mashindano ya Tusker Project Fame, amewaomba msamaha mashabiki wake kutokana na hatua yake ya kujihusisha katika maswala ya uasi ya nchini kwake.

K-Dent

K-Denk ambaye kupitia ukurasa wake wa Facebook amekuwa akiweka mitazamo yake mbalimbali kuhusiana na jitihada za waasi huko Sudan Kusini kupigania kile alichokiita ukombozi wao, ametaka mashabiki hawa kufahamu kuwa alikosea na ameamua kujirudi.

Msanii huyu kwa sasa yuko nchini Addis Ababa Ethiopia, na ameamua kuachana na maswala ya mapigano na kuongeza bidii katika shughuli za muziki na utetezi wa amani.

Tags: