Jumapili , 15th Feb , 2015

Mkali wa michano, Kala Jeremiah ameeleza mtazamo wake katika suala zima wasanii kuingia katika vyama vya siasa ambapo kwa upande wake anaona hatua hiyo si sawa.

Kala Jeremiah

Amesema ni sahihi kutokana na uwezekano wa kubanwa na kushindwa kutetea maslahi ya wananchi ambao ndio mashabiki wa kazi zao.

Tofauti na wengi wanavyofikiri, Kala ambaye amejitaja kama mwanaharakati wa kuwakilisha matatizo ya wananchi kupitia muziki wake, amesema kuwa msanii anatakiwa kuangalia maslahi ya wananchi kwanza, sababu inayomuweka kando na dili zote za kufanya maonesho katika majukwaa ya kisiasa.