Jumamosi , 7th Feb , 2015

Msanii mkongwe katika gemu ya hip hop hapa Bongo, Kalapina amesema kuwa ngoma yake mpya ya Good Time ambayo amemshirikisha Ommy Dimpoz ndani yake, imekuwa ni kazi ambayo imemletea mafanikio makubwa

Kalapina

Kalapina amesema kuwa ngoma hiyo pia imemuongezea mashabiki zaidi hususan wale wa kike kutokana na utofauti wake.

Kalapina amesema kuwa, kwa muda mrefu hakuwa amehusisha ishu ya mapenzi katika kazi zake, na baada ya kuamua kufanyakazi ya aina hiyo na kumshirikisha mwana bongo flava Ommy Dimpoz, anaweza kusema kuwa rekodi hii imekuwa ni ngoma ya hip hop inayochezwa na pia kununuliwa mtandaoni zaidi.

Kalapina amesema kuwa, kupitia kazi hiyo amegundua kuwa mapenzi humgusa kila mtu na ujumbe wake huwafikia mashabiki kwa urahisi, huku akisema kuwa kwa sasa atakuwa akifanya kazi zile tu ambazo zitakuwa zinahitajika na mashabiki, kauli ambayo inatengua misingi ya 'Ugumu" ambayo rapa huyo amekuwa nao tangu alipoanza gemu ya rap.