Alhamisi , 4th Jul , 2019

Mashabiki wa muziki wa Kanye west wamehoji kwanini amemuomba msamaha rapa mwenzake Jay Z, kwenye ngoma yake mpya ya "brothers" ambayo amemshirikisha Charlie Wilson.

Kanye West na Jay Z

Mashabiki hao wamehoji baada ya kuisikiliza na kusoma maandishi yaliyopo katika ngoma hiyo , ambayo yalikuwa yanamlenga rapa Jay Z.

Maandishi ya ngoma hiyo yanasomeka kama, "nisamehe kwa kukupoteza , nakubali kwamba nimekukumbuka ,nimekukumbuka kwenye ile familia yetu na undugu wetu, nimekumbuka kusafiri na ndege na wewe kwenda jijini Paris na kukumbatiana , na kupokea simu yako ukinipigia".

Kanye west na Jay Z wameshafanya kazi pamoja kupitia album ya "Watch The Throne" ya mwaka 2011 na kutoa ngoma kali kama Otis, n**s in paris , No church in the wild na Welcome to the jungle.

Wawili hao kwasasa hawana ukaribu kama ule wa mwanzo , na hawajaonekana wakiwa pamoja kwa muda mrefu hivi sasa.