
Picha ya Msanii Kanye West akiwaka moto jukwaani
Tukio hilo liliwashangaza watazamaji wengi waliojitokeza kwenye onesho hilo na baada ya muda mfupi tu moto huo ulizimwa na wasaidizi wake kisha akatokea mtu ambaye alivalia shela la harusi wakafunga ndoa na Kanye uwanjani hapo.
Mtu huyo anatajwa kuwa ni Kim Kardashian, Mke wake wa zamani ambaye licha ya kufikishana mahakamani kwa madai ya talaka lakini bado ameendelea kumuunga mkono Kanye kwenye masuala yake.