Jumanne , 13th Mei , 2014

Wasanii nyota mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wanaotamba kwa hivi sasa wanatarajiwa kupamba tamasha kubwa la muziki, Kili Music Tour 2014 ambalo linatarajiwa kuanza kuanza tarehe 24 mwezi huu Mjini Moshi na kuendelea katika mikoa mingine tisa.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe na baadhi ya wasanii watakaoshiriki katika ziara mwaka 2014

Akizindua tamasha hilo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, amesema lengo la Kili Music Tour 2014 ni kupeleka wasanii kwenye sehemu ambazo aina ya muziki na mitindo yao inakubalika zaidi, ili kuwapatia nafasi mashabiki kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii hawa, moja kwa moja.

Nao baadhi ya wasanii watakaoshiriki katika Kili Tour wamewataka mashabiki wao kukaa tayari kwa burudani kali kutoka kwao ambazo zitajumuisha pia kazi zao mpya ambazo hazijawahi kusikia kwenye vyombo vya habari.