Kilichomfanya Chege amtaje Vanessa kwenye namba 1

Jumanne , 30th Apr , 2019

Mkali wa Bongofleva Chege Chigunda, ambaye ameachia ngoma yake mpya 'Manjegeka' aliyomshirikisha Vanessa, amesema hawajawahi kuona msanii anajitoa kwenye collabo yake kama alivyofanya Vanessa.

Vanessa na Chege

Chege amefunguka hayo kwenye eNews ya East Africa Television, ambapo ameeleza kuwa Vanessa alifanya wimbo wao kama wa kwake kwa kuzingatia ratiba za studio mpaka wakati wa kutengeneza video pamoja na promotions baada ya wimbo kutoka.

''Sijawahi kufanya collabo na msanii akaubeba wimbo kama Vanessa, yaani kila kitu amejilipia na nguo ametoka nazo Marekani kwakweli Vanessa ni namba moja wao'', - Chege.

Mbali na hilo Chege ameongelea suala na msanii wa zamani wa TMK Bi Cheka kukosa hela ya matibabu ambapo ameweka wazi kuwa hajawahi kupanga kumsaidi ila haimanishi hana uwezo wa kufanya hivyo.

Zaidi Tazama Video yake hapo chini.