Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Kilichomtokea Msami baada ya kuachana na Uwoya

Jumapili , 18th Nov , 2018

Msanii wa Bongo Fleva na mkali wa 'kudance', Msami Baby amefunguka juu ya maisha yake ya kimapenzi yalivyo hivi sasa baada ya kuachana na muigizaji maarufu Bongo Movie, Irene Uwoya.

Msami Baby na Irene Uwoya

Akijibu swali katika 'interview' ya Friday Night Live (FNL) inayorushwa na ETV juu ya kupungua kwa umaarufu wake pamoja na kuondolewa katika listi ya wasanii wanaozungumzwa kuwa ni watanashati baada ya kuachana na Irene Uwoya, Msami amesema,

"Wakati mwingine sio kila kitu lazima ukilete katika mitandao, mimi nina bahati ya kuwa na watoto wazuri tuu na hiyo ni kawaida yangu. Anapotoka mtoto mzuri anaingia mtoto mzuri lakini sio lazima tuwe tunatoa taarifa," amesema.

"Ninachotakiwa kukileta hapa ni mziki wangu, kama natoa mziki mzuri na watu wanaupenda basi hayo maisha mengine ya mapenzi ni yapo tuu kila siku," ameongeza.

Pia msami amezungumzia juu ya tabia ya wasanii wa Bongo Fleva hivi sasa kubadilisha sana staili yao ya mavazi katika majukwaa huku staili yao ya uimbaji ikibaki kuwa ileile.

"Sio mabaya kupendeza kwenye 'show' kwasababu ni moja ya sanaa ya kuwavuta watu lakini kitu kikubwa ambacho watu wanakosea ni pale wanaposhindwa kuelewa kuwa shabiki anapokuja kwenye show amekuwa ameshakuona kwenye video jinsi unavyovaa kwahiyo anategema kuona 'perfomance' yako, na sio kwa maana ya kucheza tuu, perfomance ina vitu vingi sana".

Msami ametambulisha video yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Lingoma' ambayo ameiachia rasmi wiki hii.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja