"Kingwendu alikurupuka"-Senga

Jumatano , 5th Feb , 2020

Baada ya mchekeshaji Kingwendu kutangaza nia yake ya kuendelea kugombea Ubunge kwa mwaka huu 2020, amepingwa na mchekeshaji mwenziye Mzee Senga na kusema kwamba, Kingwendu alikurupuka.

Kushoto pichani ni Senga, kulia ni Kingwendu

Mzee Senga amesema haoni nafasi ya Kingwendu kupata Ubunge, kutokana na ugumu ambao atakaokutana nao kwenye suala zima la siasa.

"Kingwendu alikurupuka sana kutaka kuwa kiongozi, anasema safari hii amejipanga kuchukua Ubunge, sasa atamuangusha nani maana uchochoro hakuna, asije akapiga foili kwenye lami kama ilivyokuwa mwanzo wakati wenzie wanaweka gia" amesema Mzee Senga.

Kingwendu pia ameweka wazi kuwa shughuli za kampeni alizozifanya mwaka 2015, zilimfanya afilisike hadi kufikia hatua ya kuuza vitu vyake, ikiwemo gari ambalo alikuwa anatumia, kwa sababu ya kuwalipa mawakala kipindi anafanya kampeni.