
Kizz Daniel.
Staa huyo anayetamba na wimbo wake wa ''Buga'' alipaswa kutumbuiza siku ya jana katika ukumbi wa Warehouse ambao zamani ulikuwa unatambulika kwa jina la Next Door Arena.
Baada ya kushindwa kutokea ukumbini waandaji wa shughuli hiyo walikwenda polisi kuripoti, na leo amekamatwa na polisi katika hoteli aliyofikia na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay