Jumatano , 13th Jan , 2016

Rapa Kendrick Lamar ambaye amepata nafasi ya kipekee ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Barack Obama Ikulu ya Marekani, ameeleza kuwa amekuwa na mazungumzo muhimu kabisa juu ya yale yanayoendelea katika nchini Marekani.

Rapa Kendrick Lamar wa nchini Marekani

Lengo la kukutana huko ni kuweza kujadili kwa kina matatizo na suluhu na masuala muhimu ya kundi la vijana.

Kendrick ameeleza kuwa nafasi hiyo ya kukutana na Rais imemjenga kama ambavyo binafsi ameweza kujengwa kwa miongozo mbalimbali aliyopewa na wale waliomtangulia katika maisha na fani anayoifanya, akishare picha kadhaa alizopiga na Rais Obama Ikulu ya Marekani maarufu kama White House.

Kukutana na Rais Obama ni sehemu ya programu ya rapa Kendrick ambayo inafahamika kama My Brother’s Keeper ikigusia umuhimu wa watu katika jamii kushiriki muongozo wa uzoefu mbalimbali wa maisha kwa vijana wadogo.