Jumapili , 8th Jun , 2014

Wasanii wanounda kundi la Goodlyfe Mowzey Radio na Weasel wamekanusha taarifa zilizozagaa kuwa wawili hao wametengana na hawapo tena katika maelewano mazuri.

Moze Radio na Weasel TV

Wakali hao ambao hivi karibuni walikuwa mjini Kigali nchini Rwanda katika tamasha moja la muziki wamesema kuwa habari hizo ni za uzushi na zisizo za msingi wowote, huku Weasel akiweka wazi kuwa Radio ni kama kaka yake na kamwe hawezi kutengana nae.

Weasle amesema imepita takriban miaka saba wakiwa wanafanya kazi pamoja ikiwa baada ya kutengana na kaka yake Jose Chameleone hivyo hakuna utengano wa aina wowote ule.