Jumatano , 13th Dec , 2017

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkongwe kwenye game na bado anafanya vizuri zaidi, au dada wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, leo anatarajia kuachia kazi mpya maalum ambayo ni zawadi kwa ampendaye.

Kazi hiyo ambayo imetambulishwa kwa jina la 'baby', imetolewa maalum kwa ajili ya mpenzi wake Spice kama zawadi yake ya Chrismas.

Siku chache zilizopita Jaydee alipost picha ya mpenzi wake huyo huku akiwaomba mashabiki wamchagulie jina la wimbo huo ambao utakuwa maalum kwake, na siku chache baadaye kuweka kionjo cha video hiyo mpya huku ikimuonyesha akiwa na Spice.

Zaidi ya hapo Lady Jaydee ameendelea kwa kumpost mpenzi wake huku huku akimwagia sifa kedekede, kuwa ndiye tulizo la moyo wake.

Kwa mujibu wa Lady Jaydee mpaka kesho video ya wimbo huo itakuwa tayari ipo kwenye acount yake ya YouTube, hivyo amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuona kazi hiyo mpya.