Ijumaa , 24th Jul , 2015

Mwigizaji nyota Leleti Khumalo aliyevuma sana miaka ya 90 akiwa kama muhusika mkuu katika filamu ya Sarafina, pamoja na staa wa michano Mos Def, wanatarajiwa kuendesha siku ya Afrika Kusini hapa Tanzania, katika tamasha la filamu la ZIFF.

Nyota wa filamu ya 'Sarafina' muigizaji Leleti Khumalo wa Afrika Kusini

Katika wakati wake hapa nchini Leleti ambaye ni maarufu zaidi kama Sarafina, mbali na shughuli ya siku ya taifa la Afrika Kusini, katika tamasha hilo la kimataifa la filamu huko Zanzibar, atashirikiana kwa karibu kuleta burudani sambamba na kukutana na wasanii kama Vanessa Mdee, Christian Bella, Ya Moto Band, Weusi, Baby J, na Sultan King.

Ugeni huu mkubwa unatarajiwa pia kuwa ni nafasi ya kipekee kwa wasanii wa filamu hapa nchini kukutana na kubadilishana uzoefu na vilevile kutengeneza nafasi za kufanyakazi kwa pamoja.