Lina afunguka kubadili dini

Jumanne , 13th Feb , 2018

Msanii wa muziki bongo mwenye sauti ya kuvutia, Estelinah Sanga ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja, amefunguka suala la kubadili dini iwapo atatakiwa kufunga ndoa na baba mtoto wake maarufu kwa jina la mchomvu.

Wawili hao ambao wako pamoja na wanaishi pamoja huku wakiwa na imani tofauti za dini, mpaka sasa hawajafunga ndoa kuhalalisha mahusiano yao, jambo ambalo wengi wamekuwa wakihisi huenda linasababishwa na utofauti wa dini, na kutaka kujua juu ya hilo.

“Tumejizoesha kubadili dini kwa ajili ya mapenzi, lakini unajua unatakiwa kubadili dini kwa uamuzi wako mwenyewe na sio sababu ya kitu fulani”, alisikika Linah Sanga akizungumza kwenye #PlanetBongo ya East Africa Radio.

Suala hilo bado linaleta hali ya sintofahamu kama iwapo Linah atabadili dini klumfuata baba mtoto wake ambaye ni Muislam, huku yeye Linah akiwa ni Mkristu aliyetokea kwenye familia ya kichungaji.