Lulu Diva afunguka kutelekeza mtoto

Ijumaa , 12th Apr , 2019

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka juu ya tuhuma za kutelekeza mtoto akisema kwamba taarifa hizo hazina ukweli kwani hajawahi kuwa na mtoto.

Akizungumza hilo, Lulu Diva amesema kwamba suala la kuwa na mtoto halina siri, na iwapo kuna mtu anamjua mtoto aliyetelekezwa basi ampeleke ili aishi naye.

Lulu Diva aendelea kufunguka

Akiendelea kufafanua zaidi tuhuma hizo zilizoibuliwa na msanii mwenzake TID, Lulu Diva amesema kwamba hawezi kumlaumu TID kwani anazeeka, huku akimtaka kuacha kuzungumza mambo ambayo hayana uhakika kwa kuwa sio vitu alivyozoeleka kuvifanya.

“TID siwezi kumlaumu anaanza kuzeeka, amekaa muda mrefu sana kwenye game, kitu kama mtoto ni vitu ambavyo automaticaly lazima kitaonekana, Lulu ana mtoto nimtupe nimpeleke wapi,  mimi sina mtoto, kama ni ninae kwa nini nisikae na mwanangu, kitu gani kitanizuia, kama kuna mtu anasema mimi nimezaa kuna mtoto wangu amlete, nitamlea”, amesema Lulu Diva.

Lulu Diva ameendelea kusema, “T.I.D asinitafute ubaya, ameanza lini kuimba taarabu kwa sababu sio muziki wake, hi ni taarab unafanya kwa sababu unaongea kitua ambacho si kweli”.

TID aliyesema Lulu Diva ana mtoto