Alhamisi , 19th Sep , 2019

Msanii wa BongoFleva Lulu Diva "Sex Lady", leo amenyoosha maelezo kwa kile kinachosemwa kuwa anamtafutia wanawake ndugu yake Idris Sultan.

Lulu Diva na Idris Sultan

Lulu Diva ameieleza EATV & EA Radio Digital kuwa,

"Hamna ila kama akiniomba namba nampa kama anaijua namba ya mtu huwa nampa sasa sijui wanaongeaga nini labda huenda ni biashara, siwezi kuhukumu moja kwa moja lakini siwezi kumtongozea mtu yeyote mwanamke siyo Idris tu''

Lulu Diva ameongeza kusema kuwa ameshampa Idris Sultan namba nyingi tu hata za watu wa kawaida kwa sababu kuna muda mwingine huwa anakuwa na ziara yake na anahitaji wanamitindo. ameeleza Lulu Diva.

Ameendelea kusema huwa hamtafutiagi wanawake ilimradi tu lakini mara nyingi huwa anamtafutia kwa ajili ya kazi.

Aidha Lulu Diva ameeleza undugu wake na Idris Sultan ni watoto wa Baba mkubwa na mdogo japokuwa wamezaliwa mikoa miwili tofauti, Lulu Diva ni mzaliwa wa Tanga na Idris Sultan amezaliwa Arusha.

Pia msanii huyo ameogopa kumtaja mwanaume ambaye alimtongoza halafu akamkatalia kwa kuhofia watu watamjua.