Lulu Diva afunguka tatizo kubwa la Alikiba, TID

Alhamisi , 5th Sep , 2019

Mkali wa muziki wa Bongo Fleva Lulu Diva 'The Sex Lady', amesema moja ya madhaifu makubwa ya msanii Ali Kiba ni kuwa msanii huyo anashindwa kufiklia mahitaji ya mashabiki zake, kwa kuchelewa kutoa ngoma.

Lulu Diva ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV kinachoruka kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 na nusu mchana, ambapo alikuwa akijibu swali juu ya udhaifu wa wasanii watatu akiwemo Ali Kiba TID, na Vanessa Mdee.

"Udhaifu wa TID dakika 2 mbele, yaani kuna muda anakuwa rafiki na kuna wakati anakuwa adui kifupi haaminiki, ila ni mtu poa sana nampenda", amesema Lulu Diva.

"Alikiba sisi tunampenda sana na mimi shabiki yake lakini kututolea nyimbo mpaka aamue mwenyewe, sometimes tunammis lakini mtu mzuri sana hana tatizo na mtu, ila ni mtu ambaye ana'enjoy' kwenye ulimwengui wake natamani kuishi kama yeye", amesema Lulu Diva

Kuhusiana na udhaifu wa Vannesa Mdee Lulu Div amesema ni rafiki yake wa karibu kwa anafahamu ni mtu ambaye amekuwa akiumizwa mara kwa mara kwa kukosa uvumilivu.

Tazama mahojiano kamili hapo chini