Jumatano , 4th Dec , 2019

Muigizaji wa filamu hapa nchini na mjasiriamali, Shamsa Ford, amesema kwenye pochi yake kitu ambacho hakikosekani ni 'Lipshine' na kitu asichokipenda ni kuvaa nguo za ndani kwa sababu huwa zinamletea karaha.

Msanii wa filamu Shamsa Ford

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Shamsa Ford amefunguka kuwa, katika mitoko yake ya siku hutumia kiasi cha Shilingi 150,000, na kwamba anapendelea zaidi kuvaa nguo za mitumba.

"Mimi napenda mitumba ndiyo safi zaidi, kwenye nguo za mitumba napata vitu vya kipekee sana ambavyo huwezi kufanana na mtu, ila nguo zangu za ndani mara nyingi napenda kununua na kuvaa pale napokaribia kuingia 'Period' au nikiwa faragha na mpenzi wangu, sipendi kuzivaa kwa sababu huwa zinanisumbua" amesema Shamsa Ford.

Pia amesema kama akiambiwa achague kati ya mtandao wa Whatsapp na Instagram, yeye atachagua Whatsapp, kwa sababu huko kuna watu wengi ambao anawasiliana nao.