Arnold Schwarzenegger
Nguli huyo wa filamu nchini Marekani ameeleza hilo kupitia Ukurasa wake wa Twitter ambapo ameweka wazi kuwa hawezi kumpa umaarufu mtu huyo mtu badala yake anaendelea na mambo yake.
''Wengi wenu mmekuwa mkiuliza kuhusu hatua gani nitachukua, sitafungua mashtaka. Natumaini hii ilikuwa ni simu ya kuniamsha, nadhani atakuwa ameweka maisha yake kwenye njia sahihi na mimi nimechagua kuendelea na maisha yangu kwaajili ya maelfu ya wanariadha wengi niliokutana nao hapa Afrika Kusini'', amesema.
Nyota huyo wa Hollywood mwenye miaka 71, alishambuliwa kwa teke la mgongoni alipokuwa kwenye tamasha lake la Arnold Sports Event siku ya Jumamosi ambapo mtu alimrukia na kumpiga teke.
Tamasha hilo la Arnold Event huwa linahusisha michezo mbalimbali na linafanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo nchi za USA, Australia, Brasil, South Africa na Hispania.