Mabeste afikishwa polisi na mzazi mwenziye

Jumatatu , 1st Jun , 2020

Msanii Mabeste ameteka vichwa vya habari vya burudani siku ya leo Juni 1, 2020, baada ya kuitwa kituo cha Polisi Oyster Bay kwa kosa la kumchafua mitandaoni mzazi mwenziye na mkewe wa zamani Lissa.

Mabeste akiwa na mkewe wa zamani na mzazi mwenziye Lissa

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Mabeste amesema ameenda kituo cha Polisi na anasubiria hadi atakapopangiwa kwenda tena na kosa ni kumchafua kupitia wimbo wake mpya wa Back Off na kumtangazia kwa watu na kwenye vyombo vya habari kwamba mtoto aliyekuwa naye sasa hivi ni wake.

"Ishu ni kwamba nilikuwa nimeshtakiwa na mzazi mwenzangu kwamba namdhalilisha, nimeenda kusikiliza malalamiko yake ambayo anadai kwamba nimemchafua kwenye mitandao kupitia wimbo wa Back off, kuwa unamlenga yeye katika kumdhalilisha zaidi, kingine ni mtoto wake aliyempata sasa hivi, anadai natangaza kwamba ni wa kwangu kwa hiyo inamletea shida kwenye mahusiano yake" amesema Mabeste.