Jumamosi , 25th Oct , 2014

Msanii mkali wa muziki Bongo, Madee amekiri kuwa kupata connection za kufanya kolabo na wasanii wa kimataifa ni kazi ngumu japokuwa kila siku jitihada zinafanyika ili kuunganisha pamoja biashara hii ya muziki na wasanii kutoka nje ya nchi.

Madee

Madee amesema kuwa, kwa sasa wakiwa wanaongozwa na msanii Diamond Platnumz, mipango ya kuunganishwa na wasanii wakubwa kufanya nao kazi, ambayo inahitaji kuhangaika sana, inafanyika na katika siku za usoni itaanza kuzaa matunda.