Madee 'amfungia' binti yake Instagram

Friday , 21st Apr , 2017

Rais wa Manzese, Madee Seneida ameapa kutomuhusisha binti yake na mitandao ya kijamii kwa sasa bali anapambana kufanya kazi katika kuhakikisha anamtengenezea binti yake maisha na kumuwekea akiba ya pesa benk na siyo picha.

Madee

Akiwa EATV Madee amesema kuwa maisha yake binafsi hayahusiani na mitandao ya kijamii na ndiyo sababu ya kugoma kumfungulia mtoto wake akaunti ya instagram kama wasanii wengi wakubwa ulimwenguni na Tanzania kwa ujumla.

"Mimi nilijua naulizwa kwa nini sijamfungilia mtoto wangu akaunti ya benk, kumbe tu ni akaunti ya Instagram jamani.... mimi  nitamfungulia akaunti ya benki na tayari nilikwishafanya toka alipozaliwa na siyo insta, mtoto mwenyewe nakaa naye mtaani siku 15 kati ya miezi sita hizo picha nitakuwa nampiga saa ngapi, hata mastaa wanaowafungulia watoto wao inaelekea wana muda wa kutosha lakini mimi muda sina na sitaweza kusimamia hata hiyo akaunti ya instagram yake na yangu ila akikua atafanya mwenyewe" - Madee.

Katika hatua nyingine Madee amekanusha vikali tetesi za kuwa na mtoto mwingine.

"Sina mtoto mchanga, bali nina mtoto mmoja ambaye ni Sada pekee na sula kama la kuwa na mtoto siwezi kulificha kwa sababu atakua... Mbona Sada niliwaambia. Kusema nina mtoto mwingine saizi ni mapema sana ingawa nina watoto wawili ambao ni Sada na Abdul-Aziz au Dogo Janja" Madee alimaliza.