Picha Baba Levo na Wakazi
Mahakama imeamuru hivyo baada ya Baba Levo kuwasilisha kwa Mwanasheria wake kwamba alichafuliwa na Wakazi kwa tuhuma za wizi wa simu za watu Marekani
"Leo Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Imemuhukumu msanii Wakazi Kunilipa 100M"
"Nadhani mnakumbuka nilipopoteza begi la simu Uturuki Wakazi alisimama kutangaza kama nimeiba simu za watu Marekani, mbaya zaidi alianza kuyataja Makampuni ninayofanyanayo kazi kuonyesha yanafanya kazi na mwizi"
"Kwangu mimi sio jambo zuri kushitakiana Mahakamani lakini tunapaswa kutoshadadia mambo ya uongo kwa lengo la kumchafua Mtu" ameandika Baba Levo


