Jumanne , 21st Jan , 2020

Msanii wa muda mrefu kwenye BongoFleva Dully Sykes, amesema hana noma yoyote kwa mtu kumwita jina la mkongwe kwa sababu bado anaenda sawa na vijana pia anafanya mziki mzuri.

Picha ya msanii wa muziki Dully Sykes

 

Akiieleza EATV & EA Radio Digital, Dully Sykes amesema akiitwa mkongwe ni sawa kwa sababu ni jina tu na hawezi kujifananisha na vijana.

"Wasanii wengine ukiwaita wakongwe wanakataa kwa sababu wameshindwa kuendelea kufanya vizuri, kwahiyo ukimuita hivyo anaona unazidi kumkandamiza, sasa mimi kila siku nafanya vizuri, nikiitwa hivyo nachukulia sawa tu kama jina ila nafanya vizuri" amesema Dully Sykes.

Aidha ameendelea kusema "Mimi ni mkongwe ambaye nafanya vizuri mpaka leo, siwezi kujifananisha na vijana halafu nikatae ukongwe wakati nina miaka 20 kwenye tasnia ya  muziki, kama umri vile wa mtoto wa kike ambaye na yeye anamiliki wa kwake, kuzeeka ni Mungu tu ndiyo ametaka iwe hivyo, ila naenda nao sawa kama upepo ukienda huku naufuata ukirudi narudi nao" ameongeza.