Alhamisi , 7th Feb , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaongoza makundi mbalimbali ya wasanii Jijini Dar es salaam kutembelea mradi wa reli ya kisasa maarufu kama SGR.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

Msafara huo umeanzia  eneo la Stesheni Jijini Dar es salaam ambapo ilishuhudia wasanii mbalimbali wakiongozwa na kiongozi wao Steve Nyerere walijumuika pamoja kuelekea mkoani Morogoro.

Makonda amesema, "sisi tulioko kwenye Mkoa wa Dar es salaam ndiyo wanufaika wa kwanza wa mradi wa reli ya kisasa, niwashukuru wasanii wote ambao mmejitokeza leo."

"Niwaombe ndugu zetu wa Bongo Muvi muigize kwenye mradi wa reli ya kisasa ili miaka ijayo 20, 30 tukabaki kwenye historia ya ujenzi wa reli hii, unauwezo wa kupiga shoo Dodoma ukalala Mwanza." ameongeza Makonda.

Hivi karibuni akizungumza na wasanii, Makonda aliwataka wasanii kuweka kipaumbele mambo ya msingi na yenye tija ili waweze kupiga hatua za kimaendeleo.