Jumatatu , 27th Apr , 2026

Uongozi wa Klabu ya Manchester United unatarajiwa kufanya maboresho makubwa ya kikosi hicho huku ikijiandaa kuwaachia jumla ya wachezaji 13 ili kupisha ujenzi mpya wa kikosi chini ya Michael Carrick.

Wachezaji wa Manchester United

Carrick, ambaye amefanya kazi kubwa ya kuimarisha timu na kuifikisha kwenye nafasi 5 za juu, anatarajiwa kupewa rungu la kudumu na tayari mchakato wa kusafisha kikosi umeanza.

Wanaotajwa kuwa kwenye orodha ya kuondoka Old Trafford ni Casemiro ambaye ataondoka kama mchezaji huru, Marcus Rashford anatarajiwa kuuzwa baada ya kiwango bora alichokionyesha akiwa na Barcelona.

wachezaji Waliopo kwa Mkopo pamoja na Jadon Sancho, Rasmus Hojlund, na Andre Onana hawatarajiwi kurudi kikosini, huku wakitafutiwa timu za kudumu.

Wachezaji wanaopewa nafasi ndogo za kusalia ni pamoja na Manuel Ugarte, Tyrell Malacia, na Joshua Zirkzee ambao wamekuwa na wakati mgumu chini ya Carrick. Golikipa  Altay Bayındır na Radek Vítek nao mustakabali wao ukiwa gizani.

Baada ya kuwasajili mastaa kama Mbeumo, Cunha, na Sesko msimu uliopita, United sasa inaelekeza nguvu kusaka kiungo mpya wa kuziba pengo la Casemiro na kusaidiana na Kobbie Mainoo