Jumamosi , 1st Aug , 2015

Usaili wa pili wa shindano la Dance 100% (2015), umedhihirisha ubunifu na vipaji vingine leo kwa mafanikio makubwa Don Bosco Upanga, Dar es Salaam, makundi mengine matano,..

Makundi yaliyofanikiwa kuingia robo fainali kutokea hapa Don Bosco Upanga katika mashindano ya #2015Dance100

The Winners Crew, Mad Squad, The Heroes Crew, Mavuno Crew na Dream Team wakijipatia nafasi ya kuingia katika michuano.

Washindi hawa wanaungana na Team ya Shamba, The WT Crew, W.D, Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho ambao walipita kutoka usaili wa kwanza TCC Chang'ombe Temeke Jumapili tarehe 26 Julai.

Ushindani wa leo umenakishiwa na uwepo wa kundi la wasichana la Cute Babies ambao watalazimika kushiriki tena katika usaili wa mwisho Don Bosco Oysterbay wikiendi ijayo baada ya kucheza wakiwa wanne tu tofauti na masharti yanayoelekeza washiriki kuwa kundi la watu watano mpaka nane.

Majaji wa shindano kwa mwaka huu, Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen kwa ujumla wameeleza kufurahishwa kwao na namna washiriki walivyobadilika na namna wanavyojituma kulingana na masharti waliyopewa na kuzidisha chachu ya mashindano kila hatua.

Makundi mengine yaliyojitokeza leo ni Perfect Crew, The Sun Crew, Mavuno Crew, Bustani Dancers, Be Happy, na Swaga the Don ambayo alama zao hazikutosha kusonga mbele.

Usaili wa tatu na wa mwisho wa mashindano haya utafanyika Don Bosco Oysterbay siku
ya jumamosi Tarehe 8 Agosti 2015.

Dance 100% 2015 inaletwa kwako na EATV, East Africa Radio na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania “Kazi ni Kwako pia Cocacola, kinywaji rasmi cha dance 100% kwa mwaka huu.

Majaji Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen kazini.
Kundi pekee la kike Cute Babies wakiwa na watangazaji wa #2015Dance100 baada ya kufanya yao Don Bosco Upanga.