Malkia Karen afunguka kulala na Foby

Jumatano , 4th Sep , 2019

Tumepiga stori na msanii chipukizi Malkia Karen, ambaye ameeleza mambo mengi ikiwemo kuhusu kashfa za wasanii wa kike, wanaume kushindwa kumfuata na 'issue' ya kulala pamoja na msanii Foby.

Foby na Malkia Karen

Kuhusu kashfa za wasanii wa kike waliomtangulia kwenye muziki Malkia Karen ameiambia EATV & EA Radio Digital kuwa,

"Sidhani kama ni wasanii wote wanakuwaga na kashfa lakini kila mtu ana maisha yake, kila mtu ni mwanadamu, kuna vitu ambavyo wanapitia labda hawakujua kama inaweza  kuwa kashfa kwa hivyo siwezi kuwahukumu".

Malkia Karen ameendelea kusema wasanii wakiume wanaogopa kumtongoza kwa sababu baba yake anapiga mitama na watu wanamuheshimu sana na hajawahi kuingilia mahusiano yake wala kutoa maoni yoyote kuhusu anachokifanya.

Pia ametolea ufafanuzi kuhusu kumpost msanii Foby kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na 'issue' ya kulala pamoja,

"Mara ya mwisho kuonana na Foby nilikwenda naye Mbeya, ilikuwa ni lazima kulala na Foby hoteli moja kwa sababu tulikuwa kwenye show moja ila hamna kitu cha mahusiano".

Kwa sasa Msanii huyo ameachia wimbo mpya uitwao Tutoke.