Mambo 10 kuhusu Burna Boy mwaka 2019

Jumatatu , 6th Jan , 2020

Kwa wapenzi wa burudani, nadhani hakuna asiyelifahamu jina la msanii Burna Boy, kutoka nchini Nigeria barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

Msanii Burna Boy

Sasa kupitia tweet na picha ambayo ame post msanii Burna Boy, ameweka orodha ya mafanikio aliyoyapata kwa mwaka 2019, pamoja na vitu alivyovifanya kupitia kazi yake ya muziki.

1.Kuachia Album ya African Giant

2.Kupata wasikilizaji milioni 13 kwa mwezi kupitia mtandao wa Spotify na kumfanya awe msanii aliyesikilizwa zaidi Africa ndani ya mwezi mmoja.

3.Album yake ya African Giant kuingia kuwania tuzo kubwa duniani  za Grammy, katika kipengele cha Album bora duniani mwaka 2019.

4.Mambo 10 kuhusu Burna Boy mwaka 2019.

5.Album ya African Giant ndiyo Album iliyosikilizwa zaidi Africa kwa mwaka 2019.

6.Ameachia video 10 au zaidi za nyimbo zake alizozitoa mwaka 2019.

7.Amefanya show 200 na zaidi katika miji mingi duniani, ikiwemo show 70 alizofanya katika bara la Ulaya na Amerika ambapo tiketi zote ziliisha kwenye show hizo.

8.Ameshinda tuzo ya mtumbuizaji bora wa Africa kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards, pia ameshinda tuzo ya msanii bora wa kimataifa kupitia tuzo za BET Awards mwaka 2019

9.Amepewa medali ya heshima baada ya baada ya kuuza tiketi zote na kujaza uwanja wa Wembley, jijini London nchini Uingereza kupitia ziara yake ya kimuziki "African Giant Tour"

10.Ameshinda tuzo 2 kubwa Africa, ambapo amekuwa msanii bora wa Africa kupitia tuzo ya Soundcity MVP Awards na Afrimma Awards kwa mwaka 2019.