Jumatatu , 14th Mei , 2018

Ikiwa dunia imetoka kuadhimisha siku ya mama duniani hapo jana May 13, nakuletea historia fupi ya namna msanii ambaye alikuwa na mapenzi ya kupitiliza kwa mama yake alikubali kutoa uhai wake kwa ajili yake.

Anaitwa Garnet Damion Smith maarufu kama Garnet Silk, mwanamuziki wa reggae na mfuasi wa Rastafarai kutoka Jamaica, aliyezaliwa April 2, 1966 huko Machester Jamaica, alizaliwa na kulelewa na familia ya mama mmoja anayeitwa Etiga Gray akiwa na kaka zake na dada zake, huku akijihusisha na muziki akiwa na miaka 12 tu, na mpaka kuja kupata umaarufu mkubwa nchini Jamaica na duniani, kwa ngoma zake kali kama Love Is the Answer, Lord Watch Over Our Shoulders, Greensleeves na nyinginezo

Siku moja alikwenda kumtembelea mama yake nyubani kwao akiwa ameazima bastola kutoka kwa mwanasheria wake huku akiwa hajui namna ya kuitumia, baada ya nyumba yao kuvamiwa na vibaka, wakiwa wamekaa na rafiki zake nyumbani kwa mama yake Garnet, rafiki yake mmoja alimuomba amuonyeshe namna ya kuitumia, na kwa bahati mbaya ililipua mtungi wa gesi na kulipua nyumba yote.

Wakati moto unaendelea kuteketeza nyumba walifanikiwa kutoka nje, yeye pamoja na kaka zake na watu ambao walikuwa hapo, baada ya kugundua kuwa mama yake hajatoka nje na amebaki ndani, ndipo Garnet alikimbilia ndani kujaribu kumuokoa mama yake, lakni hakufanikiwa na wote wawili kufa kwenye ajali hiyo ya moto, iliyotokea mnamo Desemba 9, 1994.

Na huo ndio ukawa mwisho wa maisha yake na kuacha historia kubwa yenye ujumbe mzito wa namna ya upendo aliokuwa nao kwa mama yake, ulivyoweza kuondoa uhai wake, huku akiwa ameacha rekodi maalum ambayo alikuwa amemuimbia mama yake “Mama”, kutofanikiwa kumpa mama yake kama zawadi, kwani alikufa bila kusikia alichomuimbia.

Usikilize hapa wimbo wake wa 'mama'.