Jumatano , 28th Mei , 2014

Msanii wa filamu wa aliyepoteza maisha juzi usiku yeye na mtoto wake aliyekuwa anajifungua, Racheal Haule atazikwa siku ya kesho jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Kinondoni, baada ya mpango wa kumsafirisha kuelekea Njombe kubadilika.

Baadhi ya wasanii Bongo Movie wakiwa wamekusanyika kushughulikia mambo ya msiba.

Kwa mujibu wa shemeji wa marehemu, Bwana Issa Ahmad, Shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu zitafanyika Leaders Club Kinondoni kabla ya kuelekea makaburini kuzika mchana.

eNewz inaiombea roho ya marehemu Racheal Haule mapumziko mahala pema peponi na kutoa pole kwa wote wanaoguswa na msiba huu.